Home KITAIFA Ufaulu kidato cha nne 2025 wapanda kwa asilimia 2.61

Ufaulu kidato cha nne 2025 wapanda kwa asilimia 2.61

Na Esther Mnyika, Dar es Salama

BARAZA la mitihani Tanzania (NECTA) leo Januari 31 2026 jijini Dar es Salaam limetangaza matokeo ya kidato cha nne uliofanyika Novemba,17 2025 twakimu zinaonesha ufaulu umepanda kwa asilimia 2.61 na kufikia asilimia 94.98.

Pia amesema wanafunzi 77 wamefutiwa matokeo ya kidato cha nne kwa sababu waliandika lugha ya matusi katika skripti zao na wengine udanganyifu katika mtihani kati ya hao 47 kutoka kwenye vituo vya mtihani na 30 kutoka shule.

Akitangaza matokeo hayo Katibu Mtendaji wa NECTA, Profesa Said Mohamed amesema Jumla ya watahiniwa 595,810 walisajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha nne wakiwemo wasichana 318,910 sawa na asilimia 53.53 na wavulana 276, 900 sawa na asilimia 46.47.

Amesema watahiniwa 526,620 wamefaulu kwa kupata darajala I, II, III na IV na ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu wameongezeka wakiwa wanafunzi 255,404 sawa na asilimia 46.1.

“Jumla ya wanafunzi 569,883 walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya sekondari waliosajiliwa katika shule 5, 864 na watahiniwa na kujitegemea wakiwa 25, 927 waliosajiliwa katika vituo 813,” amesema.

Profesa Mohamed amesema kati ya watahiniwa 526, 620 waliofaulu wasichana ni 278, 108 sawa na asilimia 94.26 ya wasichana wote wenye matokeo na wavulna ni 248, 512 sawa na asilimia 95.79 ya wavulana wote wenye matokeo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here