Na Esther Mnyika,Dar es Salaam
SERIKALI imejipanga kupata wataalamu wengi zaidi ambao watasambaa katika hospitali mbalimbali nchini kwa lengo la kutoa huduma zinazohusiana na uvimbe wa ubongo na mishipa ya fahamu na kuhakikisha wataalamu wake wanapata ujuzi wa kutosha kwa lengo la kusaidia wananchi nchini.

Hayo ameyabainisha leo Febriluari, 16 2026 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa (MOI), Balozi Dk. Mpoki Ulisubisya katika mkutano wa tano wa Kitaifa na Mataifa utakaoleta watalaam wa Kimataifa ambao wataangalia saratani ya uti wa mgongo, uvimbe katika ubongo na mishipa ya fahamu.
Amesema mkutano huo ni muhimu kwao sababu utatoa fursa ya kubadilishana uzoefu na utasaidia kutoa tiba za kisasa na zilizo bora kuliko zile zilizokuwa zinatumika awali.
“Pamoja na kubadilishana mawazo kutakuwa na aina nyingine mafunzo kwa wataalam wanaoibukia wakiwemo waguuzi ambao hao watatoa huduma kwa wagonjwa wanaotoka kwenye vyumba vya upasuaji wa maradhi hayo na wauguzi hawa watakuwa watatoa huduma kwa wagonjwa mahututi ambao watakuwa wametoka katika vyumba vya upasuajii wa mishipa ya fahamu na uvimbe katika ubongo,”amesema.
Ameongeza kuwa mafunzo hayo yataambatana na mafunzo ya utengamao ambapo kwa mara ya kwanza nchini kutakuwa na madaktari wanaosimamia kazi ya utengamao. .
“Tunafanya mkakati huu kama maandalizi rasmi ya kupeleka wafanyakazi sehemu maalum ya utengamao ambayo itajengwa kule mbweni mkoani Dar es Salaam eneo ambalo linamilikiwa na taasisi yetu,”amesema.
Dk.Ulisubisya amesema mafunzo yatakayotolewa yataleta tija kwa wagonjwa watakaofanyiwa upasuaji wa mfumo wa fahamu na uvimbe wa ubongo.
Naye Mtaalamu wa Magonjwa ya Mfumo wa Fahamu kutoka MOI, Dk. Nicephorous Rutabasibwa amesema lengo la kuleta wataalamu mara kwa mara nchini ni kutaka taasisi ya MOI iwe hospitali ya kwanza Afrika itakayokuwa inatoa matibabu ya uvimbe wa ubongo.
“Kwa kila watu laki mbili ni lazima watu kumi watakuwa na matatizo ya uvimbe katika ubongo hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kujikita kwenye hilo,”amesema.
Kwa upande wake, Daktari Bingwa Mbobezi wa Ubongo, kutoka Chuo Kikuu cha Colorado cha Nchini Marekani , Profesa Ryan Ormond amesema mafunzo hayo yataambatana na mada mbalimbali za afya kwa wataalamu na wataalam wanaoibukia.

Pia amesema kutakuwa na maonesho ya vitendo katika vyumba vya upasuaji ambayo yatawasaidia wataalam kujifunza kwa vitendo.
“Uhusiano wetu na taasisi ya MOI una faida kubwa toka mwaka 2000 kwa sababu tumekuwa tukibadilishana mawazo ya kLicha ya hivyo kunawatu wamekuja katika nchini kwetu,”amesema.



