Na Mwandishi wetu
MWENYEKITI wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao, Steven Mengele maarufu kama”Steve Nyerere” amesema wanatarajia kufanya Tamasha kubwa kwaajili ya walemavu nchini na kuwapatia mahitaji muhimu mbalimbali ikiwemo wheelchair.
Akizungumza leo Machi 11 jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Mwenyekiti huyo amesema lengo la taasisi hiyo ni kusaidia jamii na wanafanya kazi na makundi mbalimbali.
Amesema lengo la Tamasha hilo ni kusoma dua kwaajili ya nchi kuendelea kuwa kisiwa cha amani na watu wote waliotangulia mbele za haki.
“Taasisi hii imefanya mambo mengi kwenye jamii na kusaidia ikiwemo kuwapatia watoto vifaa vya shule, sare na viatu kwa wanafunzi,” amesema Steve.
Amesema katika Miaka mitatu ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan wataungana na makundi mbalimbali kusaidia jamii Wamezindua rasmi leo kauli mbiu yao “mtonye mwenzako mama tena”
Ameongeza kuwa kila mwezi watakuwa wanatoa tathimini ya taasisi hiyo.
Kwa upande wake Susan Lewis maarufu kama Mama Natasha amesema Taasisi hiyo inajumuisha wasanii mbalimbali ambao wanalenga kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali ikiwemo kusaidia vifaa vya shule vua watoto .