Home KITAIFA DOYO KUGOMBEA NAFASI MWENYEKITI TAIFA ADC

DOYO KUGOMBEA NAFASI MWENYEKITI TAIFA ADC

Na Sophia Kingimali.

ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama Cha Alliance for Democract Change(ADC) Taifa Doyo Doyo ametangaza nia ya kugombea nafasi ya Uenyekiti Taifa baada ya Mwenyekiti wa Sasa Hamad Rashid Mohamed kumaliza muda wake kikatiba

Pia Scola Kahana aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Kibaha Mjini mwaka 2020 kupitia Chama hicho ametangaza nia ya kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa Ili aweze kushirikiana na Mwenyekiti Taifa kukinoa Chama hicho na kukiwezesha kuwa Chama Cha mfano

Akitangaza nia yake mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 6,2024 amesema ameona kuwa anatosha kugombea nafasi hiyo na endapo atafanikiwa atapambana Ili kuendelea kukiimarisha chama kiweze kufikia viwango vya juu na kupata uwakilishi katika maeneo mbalimbali ya nchi.

“Kutokana na uzoefu wa miaka 10 nilioupata kutoka kwa Mwenyekiti aliiyemaliza muda wake naahiidi kuyaendeleza mazuri yote hususan kuilinda katiba ya chama,”amesema.

Amesema Juni 11,2024 atachukua fomu rasmi kwa ajili ya kugombea nafasi hiyo na kuwaomba wanachama wenzake ndani ya chama itakapofika Juni 27 mwaka huku wamchague Ili aweze kufanya yote aliyokusudia na Chama kiweze kufikia viwango vya juu.

Doyo amemshukuru Mwenyekiti anayemaliza muda wake kwa kuilinda katiba ya chama aliyoitumikia kwa awamu mbili na kukubali kuachia ngazi huo ni mfano mzuri kwa kuwa wapo baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa na tabia ya kung”ang”ania madaraka

“Katikà utaratibu huu Hamad Rashid ametufundisha jambo hususan vyama vya Siasa na hili liwe somo kwa viongozi wengine kutoka vyama mbalimbali wakiwemo vizazi vipya,”amesema Doyo.

Aisha ameongeza kuwa endapo atafanikiwa kushinda nafasi hiyo atakisaidia chama kusukuma ajenda za upatikanaji wa ajira,elimu Bora,na kupata wabunge wawakilishi watakaowakilisha wananchi katikà changamoto zao bungeni .

Naye, Mwenyekiti wa Vijana Taifa Ibrahimu Pogora amempongeza Doyo kwa kutangaza Nia yake na kuahidi kushirikiana naye katikà harakati zote za uchaguzi ili kupata wadhamini Bara na visiwani

Amewataka wanachama wa Chama hicho kutambua kuwa wanadhamana na mtia Nia wa nafasi hiyo kwa kuwa Doyo si mwanachama wa kuletwa bali ni mwanzilishi wa Chama hicho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here