Home KITAIFA BOT KUTOA MIONGOZO NA KANUNI MPYA KWA AJILI YA KURATIBU WATOA HUDUMA...

BOT KUTOA MIONGOZO NA KANUNI MPYA KWA AJILI YA KURATIBU WATOA HUDUMA NDOGO ZA KIFEDHA DARAJA LA PILI.

Na Esther Mnyika@Dar es Salaam

BENKI kuu ya Tanzania (BOT)ipo mbioni kutoa miongozo na kanuni mpya kwa ajili ya kuratibu watoa huduma ndogo za kifedha daraja la pili ili kukabilina na changamoto zilizopo ikiwemo uvinjifu wa utu,sheria na maadili katika utoaji wa mikopo .

Akizungumza Juni 10,2024 jijini Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo kwa watoa huduma ndogo za kifedha daraja la pili Gavana wa BoT, Emmanuel Tutuba amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa watoa huduma daraja hilo ikiwemo ujuzi, uwezo na kubadilishana uzoefu. 

Amesema kumekuwepo na malalamiko mengi yanayotokana na vitendo vya ukiukwaji wa maadili na utu vinavyo fanywa na baadhi ya watoa huduma ndogo za kifedha hali inayo haribu biashara ya sekta ya fedha.

“Tunafahamu ipo mikopo amabayo imekuwa ikiwaumiza sana wakopaji aidha kwa kutokuja na kukosa uelewa sasa na kuita majina mabaya kausha damu, chinjachinja na majina mengineyo ili kumlinda mkopaji na mkopeshaji tumejipanga kuja na miongozo itakayosaidia kulinda utu na maadili,” amesema Tutuba.

Amesema ili kukabiloana na changamoto hizo benki kuu imeamua kuja na miongozo na kanuni zitakazo saidia kurekebisha sekta ya fedha hasa katika mikopo.

Amesema kanuni hizo zinatarajiwa kutoka mwezi julai,2024 na zitaainisha miongozo na taratibu za kufuatwa katika uendelezaji wa utoaji wa huduma ndogo za kifedha.

Ameongeza kuwa  waendesha mkopo  kuwasilisha kiwango  cha riba kwa BOT  kufuatilia  na kuweka wazi mikataba yao kisheria  na kuhakikisha ana leseni na ambae hana atachukuliwa hatua za kisheria.

“Ili kuweza kufanikisha hili Chuo cha benki kuu kimekuwa kikishirikiana na kurugenzi ya usimamizi sekta ya fedha kutoa mafunzo ya muda mfupi ambapo mafunzo hayo utolewa kwa watoa huduma ndogo za kifedha daraja la pili katika matawi yetu yote”,Ameongeza Gavana Tutuba.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Benki Kuu Dk. Nicas yabu amesema licha ya mafunzo hayo tayari wamesha fanya uelimishaji kwa watoa huduma zaid ya 1120 kwa mwaka huu.

Amesema  licha ya kuwa wameamua kufanya mafunzo mafupi kwa watoa huduma wa huduma ndogo za kifedha ili kupunguza ama kuondoa kabisa changamoto zilizopo.

Nao,baadhi ya watoa  huduma ndogo za kifedha wamesema kwa sasa ni kweli kuna baadhi yao wamekuwa wakikiuka sheria na taratibu  hivyo ni muhimu kupatiwa mafunzo hayo huku wakiwataka wananchi pia kuheshimu na kupata elimu ya mikopo ili kuondoa lawama 

Wamesema changamoto kubwa wanayokutana nayo ni uelewa mdogo kuhusu mikopo kwa wakopaji wao hali inayopelekea kuchelewa kurudisha mkopo pindi wanapokopa na wengine kushindwa kulipa kabisa.

“Sisi kwetu hii ni fursa kubwa kwani tunajifunza lakini pia kukumbushwa wajibu wetu katika kutoa huduma lakini Changamoto kubwa tunayokabiliana nayo sisi kama watoa huduma ilikuwa ni riba lakini BOT wameahidi kushughulikia lakini pia baadhi ya wateja ambao sio waaminifu,”amesema Gabriel Omende Mkurugenzi mtendaji Taasisi ya mikopo ya Uwezo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here