Home BURUDANI RAIS DK. MWINYI AAHIDI KUENDELEZA MATAMASHA YA ASILI ILI KUONGEZA IDADI YA...

RAIS DK. MWINYI AAHIDI KUENDELEZA MATAMASHA YA ASILI ILI KUONGEZA IDADI YA WATALII

Unguja

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuyaimarisha matamasha yaliyopo ikiwemo Mwaka Kogwa na kubuni matamasha mengine mapya kwa lengo la kuongeza vivutio vya utalii nchini.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo Julai, 16 2024 wakati wa akihutubia maelfu ya Wananchi waliojitokeza katika Tamasha la Mwaka Kogwa ambalo linafanyika kila mwaka Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema hatua hiyo ya Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo na Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale itasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza idadi ya watalii wanaoitembelea Zanzibar sambamba na kudumisha mila, desturi na utamaduni wa Mzanzibari.

Aidha Rais Dk. Mwinyi ametoa wito kwa viongozi wa Wilaya na Mkoa wa kusini Unguja kuhakikisha wanaweka mipango mizuri ambayo italeta manufaa kwa kutoa fursa mbalimbali za maendeleo kulingana na matamasha yaliyopo nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here