Na Esther Mnyika, Dodoma
MKURUGENZI wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA),CPA Habibu Suluo amesema wameanza kutoa vibali eneo ambalo ni jipya la usafiri wa waya lengo ni kuchochea shughuli za utalii nchini na kuhakikisha utalii unakua.

Hayo ameyasema Agosti, 8 2025 na CPA Suluo wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane ambayo kitaifa yaliyofanyika jijini Dodoma.
Amesema lengo la kushiriki Maonesho hayo ni kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu yanayofanywa na mamlaka hiyo.
“Eneo hili la usafiri wa waya wanafanyia kazi lipo kwenye sheria yetu lakini kulikuwa hakuna kanuni na kanuni imeshakamilika ipo kwenye hatua za mwisho ikasha sainiwa na kupitishwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wataendelea kutoa leseni,” amesema.
Amesema kwa kila ambaye anakuja kuwekeza katika eneo hilo la usafiri wa waya kuweza kuvutia watalii wengi nchini na kukuza uchumi.
Akizungumzia kuhusu Wadau wao wa kubwa Shirika la Reli Tanzania (TRC) ambao wao wanatoa usafiri kwa njia ya reli kwa mizigo pamoja na abiria jukumu lao kwa usafiri huo ni kutoa ithibati ile ya miundombinu inayotumika.
“Kama tunavyoona Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) inavyohusika katika usafiri wa barabara kuhakikisha barabara zimejengwa vizuri na ziko salama sisi tunasimamia ujenzi wa reli nzima pia mabehewa na vichwa vya treni vinanavyo kuja ni jukumu letu kuhakikisha vinakuja nchini vipo salama,”ameeleza CPA Suluo.
Amefafanua kuwa huwa wanakwenda kukagua vichwa hivyo na mabehewa wanavyotengeneza nje ya nchi na kabla ya kuletwa wanaangalia vina ubora kuletwa nchini ili ziweze kutumika na baada ya kufika wanakagua kwa kwa kutumia bila abiria kuangalia ubora wake wanatoa ithibati kwa TRC kuendelea kutumia vyombo hivyo vya usafiri wa reli.
Akizungumzia kuhusu usafiri wa mabasi luxury amesema LATRA hawapangi nauli zao kwa sababu wanashindana kuleta usafiri bora wao wanapanga nauli daraja la kawaida au la kati.
“Sisi jukumu ni kuhakikisha kila mtanzania anatumia huduma hii kwa kupanga nauli daraja la chini na kati ili watanzania waweze kutumia huduma hii kwa urahisi na ni huduma muhimu,” amesema.