Na Mwandishi wetu, Dodoma
MWENYEKITI wa Bodi yaMamlaka Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Profesa Sifuni Mchome amesema VETA kuhakikisha watanzania wa ngazi mbalimbali wanapata elimu na mafunzo ya ufundi ili kuwasaidia katika maisha yao ya kila siku.

Hayo ameyasema Agosti, 7 2025 Profesa Mchome alipotembelea maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane jijini Dodoma amesema mafunzo yanayotolewa na VETA yaweze kuwasaidia katika masuala ya kujiajiri na kuajiriwa na kuleta maendeleo ya Taifa na sehemu ambapo wanaishi na kufanya kazi zao.
“VETA ni ya kila mtu leo nimetembelea banda letu kuangalia shughuli mbalimbali za maonesho haya ambayo yanafanyika kila mwaka lengo kuonyesha vitu mbalimbali ambavyo vinafanyika katika maendeleo,” amesema.
Amesema wamepiga hatua katika ubunifu ameoona ubunifu wa aina mbalimbali ikiwemo wa kutumia nishati ya umeme na maonesho yajayoo kutakuwana ubunifu wa kutosha.
Ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa VETA sasa waende kwenye uzalishaji mkubwa vitu ambavyo wabuni wanatengeneza kwaajili ya matumizi mapana ya wananchi.
“Kuhakikisha tunafikia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 inawatakiwa kuwa na Taifa bunifu ambalo linazalisha kwa kiwa cha kutosha ili tuweze kufikia uchumi wa kati wa juu ambao unalenga mwaka 2050 hivyo VETA kuwa katika mchakato huu wa uhakikisha wanafikia Dira ya Taifa ya Maendeleo,” ameeleza.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ametengeneza fursa nyingi kwenye uchumi ambazo wanawake wakitumia fursa hizo kwa manufaa yao nabado hakuna ufanisi sana wanawake hawachangamkii fursa hiyo.
Amesema kuwa kuna vyuo vya VETA)hivyo kuna wanawake wangapi? wanajua umuhimu wa kupata elimu ya ufundi na wanachukua hatua ya kupata elimu hiyo.
“Nammshukuru Mkurugenzi Mkuu wa VETA kwa kuridhia na kuelewa kuwa wanawake wapate fursa ya kupata mafunzo na ujuzi ambao unawakomboa kiuchumi,”amesema.
Aidha ametoa wito kwa wanawewake ambao hawajatumia fursa hiyo bado ipo na ufundi ni ujuzi ambao unakupa haraka maarifa ya kuweza kufanyia kazi na kupata faida.