Dodoma
TAASISI ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) inashiriki katika Wiki ya Afya kitaifa 2025 inayofanyika jijini Dodoma, ambapo wananchi watapa huduma za matibabu ya kibingwa ya mifupa, ubongo, mgongo, mishipa ya fahamu na ushauri wa kitaalam.

Uzinduzi wa wiki hiyo umefanyika leo Aprili 4, 2025 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Conventional Center Jijini Dodoma, ambapo mdahalo maalam umefanyika pamoja na utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi.
Afisa Muuguzi kutoka MOI, Magreth Kumpuni amesema wanachi watakaotembelea banda la MOI watapata fursa ya matibabu ya kibingwa ya mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu.

“Tunatoa ushauri kuhusu huduma za kibingwa za Mifupa, Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu pamoja na maswala ya magonjwa ya ndani na mazoezi tiba,”amesema Magreth na kuongezea
“Watalaam wapo wa kutosha wabobezi na tupo tayari kutoa huduma bora kwa wakazi wa Dodoma”
Wiki ya Afya Kitaifa 2025 imeanza leo Aprili 4 na itafikia tamati Aprili 08, 2025 ambapo ushauri na elimu utatolewa bure.